Saturday, May 4, 2013
MAZEMBE KATIKA KIBARUA KIZITO DHIDI YA PIRATES.
KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC leo watakuwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha wanabaki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika pale watakapoikaribisha Orlando Pirates ya Afrika Kusini jijini Lubumbashi. Katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili wa michuano hiyo uliochezwa jijini Johannesburg April 20 mwaka huu Mazembe walijikuta wakikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka Pirates. Sare, kufungwa au wakishinda kwa bao 1-0 kwenye mchezo huo Mazembe itajikuta ikiyaaga mashindano mapema na hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufanya hivyo katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Mara ya mwisho Mazembe kushindwa katika hatua za mwanzoni za michuano hiyo ilikuwa mwaka 2007 wakati walipotolewa na FAR Rabat ya Morocco kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye mechi za mikondo miwili walizokutana.
No comments:
Post a Comment