Thursday, May 2, 2013
ILIKUWA NI BAHATI KUCHEZA NA bARCELONA BILA KUWEPO MESSI - HEYNCKES.
MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Jupp Heynckes anaamini kuwa kikosi chake kilipata bahati kwakuwa mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi hakuwemo katika kikosi hicho kitendo ambacho kilipelekea timu hiyo kushinda kwa mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Camp Nou. Mshambuliaji huyo wa kimataifa alikuwa katika benchi akitizama mabao ya Arjen Robben, bao la kujifungala Gerard Pique na Thomas Muller yakiididimiza timu hiyo kwa jumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya walizokutana. Wakati Heynckes akisifu umakini wa kikosi chake katika mechi hiyo ya marudiano lakini amekiri kuwa wapinzani wao walikuwa tofauti bila ya kuwepo nyota wao Messi. Kocha huyo amesema hakuna mtu aliyetegemea kuwa kikosi chake kingeibuka na ushindi wa mabao 7-0 katika mechi mbili walizokutana lakini pamoja na hivyo huwezi kusema zama za Barcelona zimekwisha kwasababu waliwakosa nyota wao wengi ambao ni majeruhi.
No comments:
Post a Comment