Friday, July 19, 2013

CAMEROON YAIANGUKIA FIFA.

MAOFISA wa serikali wa Cameroon wamefanya mazungumzo na rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter. Hatua hiyo imekuja kufuatia nchi hiyo kuamua kujisalimisha wenyewe kufuatia kufungiwa na shirikisho hilo kushiriki michezo ya kimataifa mapema mwezi huu. FIFA ilithibitisha katika mtandao wake kuwa Blatter alipokea ugeni kutoka serikali ya Cameroon katika makao makuu ya shirikisho hilo yaliyoko huko Zurich, Switzerland na moja mambo ambayo yalizungumzwa ni pamoja na maendeleo ya soka la nchi hiyo pamoja na adhabu ya kufungiwa waliyopewa. Wawakilishi hao walimhakikishia Blatter ushirikiano kutoka katika serikali ya nchi hiyo katika kutatua tatizo hilo ambalo lilipelekea Shirikisho la Soka la nchi hiyo-Fecafoot kufungiwa.

No comments:

Post a Comment