Monday, July 15, 2013
GAY, POWELL WAKUTWA NA HATI YA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU.
UKIWA umebakia mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa mashindano ya riadha ya dunia yanayotarajiw akufanyika jijini Moscow, tasnia ya riadha za mbio fupi imekumbwa na aibu nyingine baada ya Tyson Gay wa Marekani na Asafa Powell wa Jamaica kukutwa hatia ya kutumia dawa zilizokatazwa michezoni. Gay, ambaye ni mwanariadha wa pili kwa kuwa na kasi kubwa ya kukimbia katika mbio za mita mia moja, amesema anajiondoa kwenye mashindano ya dunia ya riadha yanayotarajiwa kufanyika mjini Moscow mwezi ujao. Huku Powell, ambaye alishikilia rekodi ya mbio za mita 100 hadi ilipovunjwa na Usain Bolt mwaka 2008, yeye amekanusha kuwa alitumia dawa hizo makusudi. Mwanariadha mwenzake wa Jamaica Sherone Simpson pia amepatikana na hatia ya kuzitumia dawa hizo za kusisimua misuli.

No comments:
Post a Comment