Saturday, July 13, 2013

MASHABIKI BADO HAWAJAONA UBORA WA RONALDO - PEREZ.

RAIS wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ana uhakika kuwa mashabiki wa klabu hiyo bado hawajaona kiwango cha juu cha mchezaji bora wa duniani, Cristiano Ronaldo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 28, bado hajasaini mkataba mpya zaidi ya ule unaomalizika mwaka 2015 na klabu hiyo hivyo kuzua tetesi kuwa anaweza kutimkia Manchester United katika kipindi hiki cha usajili au Monaco ya Ufaransa. Hata hivyo kutosaini mkataba mpya kwa nyota huyo kunaonekana kutomnyima usingizi Perez ambaye amesisitiza kuwa mshambuliaji huyo ataendelea kuwepo hapo kwa miaka mingi ijayo. Perez amesema Ronado ni kama kioo cha kikosi cha Madrid kutokana na kipaji cha hali ya juu alichonacho na kudai kuwa bado mashabiki hawajaona kiwango chake cha juu.

No comments:

Post a Comment