Thursday, July 18, 2013
NAHESHIMU UAMUZI WA FABREGAS - WENGER.
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa hategemei kumsainisha Cesc Fabregas katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi kutokana na kiungo huyo kuamua kubakia kwa mwaka mmoja zaidi katika klabu ya Barcelona. Arsenal walimuuza Fabregas kwa euro milioni 29 kwa mkataba wa kupewa kipaumbele cha kumsajili tena wakati alipomuuza kwa mabingwa wa soka nchini Hispania, Barcelona miaka miwili iliyopita. Lakini pamoja na Manchester United kujaribu kumnyakuwa kiungo huyo kwa kumtengea kitita cha paundi milioni 30 Jumatatu, Wenger anaamini kuwa hahitaji kuweka ofa yoyote mezani ili kumzuia nahodha wake huyo wa zamani kwenda Old Traford. Wenger amesema kiungo huyo amamua kubakia Barcelona kwa mmoja zaidi na kudai kuwa wana mawasiliano naye hivyo wako macho kusubiria uamuzi wake baada ya hapo lakini kwasasa wachezaji wengine wa kuangalia ili kujaribu kuongeza nguvu katika kikosi chake. Fabregas amekuwa akipata tabu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Barcelona mwaka 2011 lakini kuuzwa kwa chipukizi Thiago Alcantra kwenda Bayern Munich kunatoa nafasi huru kwa mchezaji huyo kuwa chaguo la kwanza la kocha Tito Vilanova kwasasa.
No comments:
Post a Comment