PELLEGRINI AIKACHA MAN CITY KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA KIFAMILIA KWAO CHILE.
KLABU ya Manchester City imetangaza kuwa meneja wake Manuel Pellegrini amekiacha kikosi chake ziarani Afrika Kusini na kurejea nchini kwao Chile kwasababu ya matatizo ya kifamilia. Msaidizi wake Brian Kidd ndiye alichukua mikoba ya kuisimamia timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Amazuli jijini Durban ambao walichapwa kwa mabao 2-0. Huo unakuwa mchezo wa pili kwa City kufungwa katika ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya waliyoianza huko huko Afrika Kusini kabla ya kuondoka kuelekea Hong Kong Jumapili. Haijawekwa wazi ni muda gani Pellegrini ambaye amechukua mikoba ya Roberto Mancini mwezi uliopita atautumia kumaliza matatizo yake ya kifamilia.
No comments:
Post a Comment