VERON ATUNGUA DALUGA ZAKE NA KUREJEA UWANJANI.
NAHODHA wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, Juan Sebastian Veron ameamua kurejea tena katika ulingo wa soka kwa kucheza msimu katika klabu ya Estudiantes huku mshahara wake ukienda kusaidia klabu ya watoto ya La Plata. Veron ambaye alikuwa katibu wa ufundi na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo msimu uliopita, amesaini mkataba mpya kama mchezaji ambao utamalizika Juni mwakani. Veron mwenye umri wa miaka 38 amesema kuwa hadhani kama yuko katika kiwango kama alichokuwanacho mwaka 2009 waliposhinda Libertadores Cup lakini anahamasika kwasababu anapenda kucheza soka. Kiungo huyo wa zamani wa klabu za Lazio na Manchester United ambaye alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya mgongo alistaafu mwaka mmoja uliopita.
No comments:
Post a Comment