Monday, August 5, 2013

BOLT APANIA KUREJESHA TAJI LAKE KATIKA MBIO ZA MITA 100 ALILOPOTEZA MWAKA 2011.

MWANARIADHA nyota wa mbio fupi, Usain Bolt amedhamiria kutobweteka kutokana na kukosekana kwa mahasimu wake wakati atakapojaribu kurejesha tena taji la mbio za mita 100 alilopoteza miaka miwili iliyopita. Bolt ambaye alitetea medali zake za olimpiki mwaka uliopita, amesema baada ya kutua jijini Moscow kwa ajili ya mashindano ya raiadha ya dunia kuwa haogopeshwi na kilichotokea jijini Daegu mwaka 2011 wakati alipoenguliwa kwa kuanza kukimbia kabla ya wenzake. Zikiwa zimebakia siku sita kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, Bolt amesema madhumuni makubwa yam bio za mita 100 za mwaka huu atazoshiriki ni kuhakikisha anarejesha taji lake na kwa maandalizi aliyopata hana shaka katika hilo. Mahasimu wa Bolt wa karibu katika mbio hizo Tyson Gay wa Marekani na Asafa Powell wa Jamaica hawatashiriki baada ya kushindwa vipimo vya dawa zilizopigwa marufuku wakati mjamaica mwingine Yohane Blake atashindwa kutetea taji hilo kwasababu ya majeraha.

No comments:

Post a Comment