Monday, August 5, 2013

NEYMAR ASUMBULIWA NA TATIZO LA UPUNGUFU WA DAMU.

MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Barcelona, Andoni Zubizarreta amedai kuwa pamoja na mshambuliaji wao nyota Neymar kusumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu kwao sio suala linalowatia mashaka kwa sasa. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye alijiunga na Barcelona akitokea Santos kwa ada ya euro milioni 57 katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi, aligundulika kuwa na tatizo hilo la upungufu wa damu ambalo linahisiwa kusababishwa na vipimo vingi vya damu alivyofanya katika siku za karibuni. Lakini Zubizarreta alisisitiza kuwa hali hiyo ya Neymar mwenye umri wa miaka 21 ni kitu ambacho madaktari wa klabu wanaweza kukimaliza na sio cha kuleta wasiwasi sana kuhusu kiwango chake. Zubizarreta amesema watajaribu kumsaidia ili kuhakikisha anakuwa katika afya njema kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi a,bapo Barcelona wataanza kutetea taji lao kwa kuchuana na Levante katika Uwanja wa Camp Nou Agosti 18 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment