Monday, August 5, 2013

DROGBA AENDELEA KUINYANYASA ARSENAL.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ivory Coast na timu ya Galatasaray ya Uturuki, Didier Drogba ameendelea kuinyanyasa klabu ya Arsenal baada ya kuifungia klabu yake mabao yote mawili kwenye ushindi wa 2-1 katika Kombe la Emirates jana. Drogba alikuwa amejenga tabia ya kuifunga Arsenal kila wanapokutana nayo wakati akiwa Chelsea na aliendeleza wimbi hilo jana baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba katika kipindi cha pili kwa kuisawazishia na kuifungia bao la ushindi timu yake katika fainali michuano hiyo inayoshirikisha timu nne. Kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Arsene Wenger inatabidi kijilaumu chenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi walizokuwa wamepata na ukosefu huo wa umakini kwenye umaliziaji ndio unaosababisha kocha huyo kupambana kujaribu kumuongeza Luis Suarez ili kuimarisha safu ya ushambuliaji. Wenger mpaka sasa amefanya usajili mmoja pekee wa mshambuliaji kinda Yaya Sanogo mwenye umri wa miaka 20 kutoka klabu ya AJ Auxerre ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment