MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Paul Gascoigne maarufu kwa jina la Gazza ametozwa faini ya paundi 1,000 kwa kosa la kufanya vurugu akiwa amelewa katika kituo cha treni. Akisimama mbele mahakama ya Stevenage, Gazza alikiri kumshambulia Jack Sherrington katika kituo cha treni cha Hertfordshire katika tukio lililotokea Julai 4 mwaka huu. Mashitaka mengine ya kumshambulia mke wake wa zamani Sheryl Gascoigne yaliyokuwa yakimkabili Gazza yaliondolewa. Tukio hilo la kumshambulia Sherrington limetokea ikiwa ni wiki chache zimepita toka nyota huyo wa zamani wa klabu ya Newcastle, Tottenham na Rangers kutoka katika kliniki ya kutibu maradhi ya ulevi wa kupindukia nchini Marekani. Gazza mwenye umri wa miaka 46 alikuwa akisafiri kutoka Newcastle kwenda London kwa treni ambapo alishuka Stevenage na kuanza kutembea kandokando ya reli kabla ya wasamaria wema akiwemo Sherrington kujaribu kumuondoa baada ya kumuona akiwa amelewa na kuanza kuwashambulia.
No comments:
Post a Comment