LEONARDO ALAUMU SHIRIKISHO LA SOKA LA UFARANSA KUCHANGIA KUJIUZULU KWAKE.
 |
Leonardo |
MKURUGENZI wa michezo wa zamani wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Leonardo amedai kuwa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa ndilo lililomlazimisha kujiuzulu nafasi yake. Leonardo alijiuzulu Julai mwaka huu ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kusimamishwa kutokana na kumsukuma mwamuzi wakati akielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo katika mechi ya mwishoni mwa msimu uliopita. Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Brazil, amesema amekuwa kiongozi wa mipango yote ya PSG na shirikisho hilo limefanya kazi yake kuwa ngumu kutokana na adhabu waliyompa. Mei mwaka huu Leonardo alifungiwa miezi tisa kwa kosa la kumpiga kikumbo mwamuzi Alexandre Castro lakini adhabu hiyo iliongezwa baadae mpaka Juni mwakani baada ya kushindwa rufani kupinga adhabu ya aliyopewa kwanza.
No comments:
Post a Comment