Monday, January 13, 2014

AUSTRALIA OPEN: DJOKOVIC, SERENA WASONGA MBELE, VENUS MWAKA WA TABU...

BINGWA mara saba wa michuano ya Grand Slam mwanadada Venus Williams amepuuza mazungumzo ya kustaafu pamoja na kuenguliwa mapema katika michuano ya wazi ya Australia na Ekaterina Marakova wa Urusi. Venus mwenye umri wa miaka 33 aliondoshwa na Marakova anayeshika nafasi ya 22 katika orodha za ubora duniani kwa 2-6 6-4 6-4 ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka 2006 kwa Mmarekani huyo kuondoshwa katika mzunguko wa kwanza. Pamoja na hayo Venus amekanusha kustaafu mchezo huo na kudai kuwa anatarajia kurejea tena nchini Australia mwakani kwasababu bado anapenda kucheza michuano mikubwa kama hiyo. Michezo mingine iliendelea tena leo ambapo dada Venus, Serena Williams alifanikiwa kuanza vyema michuano hiyo kwa kumchabanga Ashleigh Barty wa Australia kwa 6-2 6-1. Kwa upande wa wanaume bingwa mtetezi wa michuano hiyo Novak Djokovic naye alifanikiwa kutinga mzunguko wa pili kwa kumtandika Lukas Lacko wa Slovakia kwa 6-3 7-6 6-1.

No comments:

Post a Comment