Monday, January 13, 2014

ETO'O AONGOZA UTAJIRI KWA WACHEZAJI WA KIGENI UINGEREZA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Chelsea, Samuel Eto’o ametajwa kuwa mchezaji wa kigeni tajiri zaidi katika Ligi Kuu nchini Uingereza akiwa na utajiri unafikia kiasi cha dola milioni 64. Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na kampuni moja ya Singapore, nyota wa Manchester United Ryan Giggs ambaye anatoka Wales ndio anayeshika nafasi ya pili katika orodha hiyo akiwa na utajiri unaofikia dola milioni 45. Wengine ni Fernando Torres wa Hispania na klabu ya Chelsea mwenye utajiri wa dola milioni 42 akifuatiwa na nyota kutoka Ivory Coast anayecheza Manchester City, Yaya Toure mwenye utajiri wa dola milioni 41 huku tano bora ikifungwa na Muargentina Sergio Aguero wa City mwenye kitita cha paundi milioni 39. Pamoja na ligi hiyo kudaiwa kutekwa na wachezaji wa kigeni, utafiti huo ulibainisha kuwa utajiri wa jumla wa wachezaji wazawa wanaongozwa na Wayne Rooney mwenye utajiri unaofikia kiasi cha dola milioni 73.

No comments:

Post a Comment