Sunday, January 12, 2014

OXLADE-CHAMBERLAIN ANA UWEZO SAWA NA GERRARD - WENGER.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha Alex Oxlade-Chamberlain ana uwezo sawa na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Liverpool Steven Gerrard. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 hajakuwepo katika kikosi cha Arsenal toka katika mechi ya ufunguzi ya ligi dhidi ya Aston Villa baada ya kuumia goti lake la kushoto. Wenger amesema pamoja na kuumia huko kinda huyo alikabili changamoto hiyo na kuhakikisha anafanya bidii ili aweze kurejea tena uwanjani hatua ambayo amefanikiwa. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa uwezo Chamberlain anapokuwa uwanjani haotofautiani sana na mkongwe Gerrard na kama akiendelea na bidii kama hivi sasa hakuna shaka anaweza kuvaa viatu vyake siku sijazo.

No comments:

Post a Comment