Sunday, January 12, 2014

FERGUSON HAPASWI KULAUMIWA.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema Sir Alex Ferguson hapaswi kulaumiwa kwa Manchester United kushindwa kufanya vizuri msimu huu. United ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Uingereza wamekuwa wakisuasua chini meneja mpya David Moyes ambapo hivi sasa timu hiyo inashika nafasi ya saba huku wakiwa wameshang’olewa katika michuano ya Kombe la FA. Ferguson amekuwa akihudhuria katika kila mechi ya United akiwa kama mtazamaji lakini Wenger hadhani kama kocha huyo wa zamani anapswa kulaumiwa kutokana na matokeo yasiyo ya kuridhisha ya timu hiyo. Wenger amesema Ferguson amekaa miaka 27 na timu hiyo hivyo anapokwenda kutizama mechi zao hakuna kibaya lakini tatizo kubwa liko kwa wachezaji wanaokuwa uwanjani ambao ndio wanaweza kushinda mechi. Wenger aliendelea kudai kuwa wanaopaswa kulaumiwa ni wachezaji kwa kushinda kusimama na kuhakikisha wanatetea taji lao.

No comments:

Post a Comment