MARA baada ya kutua salama nchini Uturuki na kufikia Hoteli ya Sueno Beach Side eneo la Manavgat pembezoni kidogo mwa jiji la Antalya kikosi cha timu ya Yanga kimeanza mazoezi rasmi asubuhi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu pamoja na mashindano ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo Baraka Kizuguto Yanga chini ya cha wake msaidizi Charles Boniface Mkwasa ilianza moja kwa moja mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na duru hilo la pili.
Kizuguto amesema hoteli waliyofikia Yanga ina hadhi ya nyota tano huku kukiwa na jumla ya vyumba 760, mabwawa ya kuogelea, viwanja viwili vya mpira vya mazoezi kimoja kikiwa na nyasi za kawaida na kingine nyasi za bandia.
Young Africans inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya Ankara Sekerspor iliyopo Ligi Daraja la Kwanza nchini Uturuki. Aidha timu ya Sivasspor iliyopo Ligi Kuu nchini Uturuki inayonolewa na mchezaji wa zamani Real Madrid na timu ya Taifa ya Brazil Roberto Carlos pia imeweka kambi katika hoteli ya Sueno na leo asubuhi kabla ya Young Africans kuanza mazoezi waliweza kupiga picha ya pamoja na gwiji huyo.
No comments:
Post a Comment