KLABU ya Manchester United imeanza mazungumzo na Sporting Lisbon juu ya kumsaini kiungo mkabaji William Carvalho. Kocha wa United, David Moyes amemtambulisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kama mchezaji muhimu zaidi katika usajili wake wa msimu ujao na tayari imewasilisha maombi ya kumsajili Sporting. Klabu ya Sporting inaweza kumuuza mchezaji huyo mzaliwa wa Angola kwa kiasi cha paundi milioni 29, lakini United inafikiri thamani yake si chini ya paundi milioni 4. Moyes amepania kuimarisha kikosi chake mwishoni mwa msimu huu kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia hivyo kuna uwezekano wa kutoa fedha zaidi kuliko thamani ya wachezaji wanaowahitaji.

No comments:
Post a Comment