HATIMAYE mfanyabiashara bilionea wa Afrika, Aliko Dangote anajipanga kutimiza ahadi yake ya kutoa kitita cha dola milioni moja kwa timu ya taifa ya Nigeria iliyoshinda michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka jana. Hatua hiyo imekuja kufuatia nahodha wa Super Eagles Vincent Enyeama kuulizia hadharani kitita hicho walichoahidiwa baada ya kuona kimya kimezidi. Dangote aliiambia BBC kuwa walikuwa wakisubiria maofisa soka wa Nigeria kwenda kuchukua fedha hizo lakini hakuna yoyote aliyewaandikia hivyo wameamua kuwaandikia wao na kuomba akaunti za benki za wachezaji ili waweze kuwaingizia pesa zao haraka. Tajiri huyo ambaye anaongoza makampuni ya Dongote Group anahesabika kama mtu tajiri zaidi barani Afrika huku akishika nafasi ya 25 duniani kwa mujibu wa orodha za matajiri zilizotolewa na gazet la Forbes mwaka jana, akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia dola bilioni 25.

No comments:
Post a Comment