UEFA KUIWEKA BAYERN KIKAANGONI.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limefungua mashitaka ya kinidhamu dhidi ya klabu ya Bayern Munich kutokana na mabango yaliyokuwa yakionyeshwa wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal Jumanne. UEFA pia limeifungulia mashitaka mengine klabu yao ya kuchelewesha kuanzwa kwa mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1. Bango la kwanza lilikuwa likionyesha kampeni ya kutaka Kosovo itambuliwe na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA wakati lingine lilikuwa na maneno na picha za kudhalilisha. Kosovo ilitangwa kuwa taifa huru na kujitoa na Serbia miaka sita iliyopita lakini hawajawa wanachama wa UEFA wala FIFA ingawa hata hivyo wanaruhusiwa kucheza mechi za kimataifa za kirafiki na nchi nyingine huku wakinyimwa kutumia bendera au wimbo wao wa taifa. Kamati ya nidhamu ya UEFA ya UEFA inatarajia kusikiliza kesi hiyo Machi 20 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment