Wednesday, March 5, 2014

MESSI HAHITAJI KOMBE LA DUNIA ILI AWEZE KUWA MCHEZAJI BORA - MARADONA.

NGULI wa soka nchini Argentina, Diego Maradona amesema nyota wa Barcelona Lionel Messi hahitaji kushinda medali ya Kombe la Dunia ili aweze kuhesabiwa kama mmoja wa wachezaji bora kuwai kutokea. Maradona aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kilichonyakuwa Kombe la Dunia nchini Mexico mwaka 1986 amedai nyota huyo haitaji Kombe la Dunia ili kuwa mchezaji bora duniani. Maradona amesema kama akishinda Kombe la Dunia litakuw ajambo zuri kwa Argentina na kwake mwenyewe lakini hata akilikosa haiwezi kuondoa ubora wake kutokana na mafanikio aliyopata. Argentina ambao wameshinda taji la Kombe la Dunia mara mbili wanatarajiwa kucheza na Romania mechi ya kirafiki itakayochezwa jijini Bucharest baadae leo.

No comments:

Post a Comment