Wednesday, March 5, 2014

PIQUE AMUITA PUYOL MALAIKA ALIYETUMA KUWALINDA.

BEKI wa klabu ya Barcelona Gerard Pique amesema Carles Puyol amekuwa kama malaika mlinzi katika timu hiyo na amesikitishwa na taarifa kuwa ataondoka Camp Nou mwishoni mwa msimu. Beki huyo mwenye umri wa miaka 35 amekuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kwa kipindi cha zaidi ya muongo mmoja lakini jana alitangaza nia yake ya kuondoka kwa mabingwa hao wa La Liga mwishoni mwa msimu huu ambapo mkataba wake unamalizika. Pique ambaye alirejea Barcelona akitokea Manchester United mwaka 2008 aliandika barua ya wazi katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook akielezea kuguswa na taarifa hizo za kuondoka kwa Puyol. Nyota huyo amesema anajua wakati umefika wa Puyol kuondoka lakini ngumu kukitizama kikosi cha Barcelona bila muongozo wa mkongwe huyo. Pique amesema atamkumbuka Puyol kwa mengi hususani mazungumzo yao katika vyumba vya kubadilishia nguo, ushauri na umahiri wake pindi awapo uwanjani.

No comments:

Post a Comment