TUME ya kitabibu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA imetangaza kuwa hakuna mchezaji yoyote kati ya waliopimwa aliyekutwa ametumia dawa za kusisimua misuli ambazo zimekatazwa michezoni. Ofisa tabibu mkuu wa FIFA, Jiri Dvorak aliwaambia waandishi wa habari kuwa wachezaji wote 736 walioshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu walipimwa kabla ya wakati michuano ikiendelea. Dvorak amesema walianza zoezi hilo kuanzia Machi mwaka huu mpaka wakati wa kuanza michuano hiyo Juni 12 na katika vipimo zaidi ya 1,000 na vingine 232 wakati wa mashindano yakiendelea hawajapata tatizo lolote. Tabibu huo aliendelea kudai kuwa katika vipimo vyote hivyo hawajakuta chembechembe zozote za dawa ambazo haziruhusiwi kutumiwa na wanamichezo.
No comments:
Post a Comment