KLABU ya AS Roma imeanza mazungumzo na wawakilishi wa Samuel Eto’o jana baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Ashley Cole. Eto’o mwenye umri wa miaka 33 ni mchezaji huru toka aondoke Stamford Bridge na tayari amepata ofa kutoka China na Uturuki lakini mwenyewe anataka kurejea nchini Italia. Katika mazungumzo hayo nyota huyo anatarajiwa kupunguziwa mshahara wake kwa kiasi cha paundi milioni tatu ikiwemo na posho. Kama akifanikiwa kutua Roma atakuwa amejiunga na mchezaji mwenzake kutoka Chelsea, Cole aliyesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo huku ikiwa ni mara ya pili kwa nyota huyo kurejea nchini Italia baada ya kuitumikia Inter Milan kati mwaka 2009 na 2011.
No comments:
Post a Comment