Tuesday, July 8, 2014

OBI MIKAEL MGUU NDANI MGUU NJE CHELSEA.

KLABU ya Chelsea inajipanga kumuachia kiungo wa kimataifa wa Nigeria, John Obi Mikael. Klabu inajipanga kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba pamoja na meneja Jose Mourinho kuwa tayari ameshatumia kiasi cha paundi milioni 60 katika usajili majira haya ya kiangazi kwa kuwachukua Cesc Fabregas na Diego Costa. Inaaminika kuwa Mourinho anahitaji kuongeza nguvu zaidi katika safu ya kiungo kufuatia kutofanya vyema katika msimu wa 2013-2014. Obi Mikel ambaye alipoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha Chelsea kwa Nemanja Matic, kuna hati hati ya kubakia kiangazi hiki kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Uingereza.

No comments:

Post a Comment