Thursday, July 3, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: HAKUNA MATAIFA MAKUBWA KATIKA HIVI SASA - BLATTER.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ameyapongeza mataifa madogo kisoka kwa kuadhibu mataifa makubwa katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil. Kauli hiyo ya Blatter imekuja wakati wa mapumziko wa michuano hiyo kabla ya kuanza kwa hatua ya robo fainali hapo kesho. Timu zote nane zilizotinga hatua hiyo katika michuano ya mwaka huu ndio zilizokuwa vinara wa makundi yao huku timu nne zikifuzu kutoka bara la Ulaya na nne kutoka bara la Amerika Kusini. Blatter amesema soka limekuwa limekuwa kinyume na ilivyokuwa huko nyuma na imekuwa vigumu kutabiri kuwa mataifa Fulani yanaweza kufika mbali kutokana na jinsi walivyokaribiana kiviwango. Michuano ya mwaka huu imeshuhudia mataifa makubwa katika ulimwengu wa soka kama mabingwa watetezi Hispania, Uingereza na Italia wakibwagwa katika hatua za mwanzo za michuano hiyo. Hatua ya robo fainali inaaanza kutimua vumbi kesho ambapo Ufaransa itajitupa uwanjani kumenyana na Ujerumani katika mchezo wa kwanza utakaochezwa saa moja usiku kabla ya kufuatiwa na mchezo kati wenyeji Brazil na Colombia utakaofuatia baadae ambapo washindi watakutana katika hatua ya nusu fainali.

No comments:

Post a Comment