Thursday, July 3, 2014

URENO IMESHINDWA KWASABABU YA KUMTEGEMEA RONALDO - QUARESMA.

WINGA mahiri wa klabu ya FC Porto Ricardo Quaresma ameilaumu Ureno kwa kumtegemea moja kwa moja nahodha wao Cristaino Ronaldo na kudai kuwa ndio chanzo cha timu hiyo kuenguliwa mapema katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil. Ureno waling’olewa katika michuano hiyo kwenye hatua ya makundi baada ya kuchapwa mabao 4-0 na Ujerumani, kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Marekani na kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya mwisho dhidi ya Ghana. Ronaldo alikuwa katika msukumo mkubwa wa kuhakikisha anaisaidia timu yake pamoja na kutokuwa fiti kwa asilimia 100. Quaresma ambaye aliachwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa Ureno wlaioshiriki michuano hiyo pamoja na kuwa na msimu mzuri kwa timu yake amesema taifa lilitegemea makubwa sana kutoka kwa Ronaldo na kuwa kikosi kizima hakikuwa kizuri. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa haikupaswa kumtegemea sana Ronaldo kwani hachezi peke yake anapokuwa uwanjani anahitaji msaada wa wachezaji wenzake awapo uwanjani.

No comments:

Post a Comment