MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone ametamba kuliziba pengo la mshambuliaji wake nyota Diego Costa aliyetimkia Chelsea. Kocha huyo amesema kwasasa Costa yuko mahali alipokuwa akihitaji na anafurahi na kumtakia kila kheri katika timu yake hiyo mpya. Simeone aliendelea kudai kuwa wakati nyota huyo akiwa Atletico amekuwa akitoa kwa nguvu na mara zote amekuwa akiwapenda wachezaji wa namna hiyo. Amesema kwasasa Costa yuko katika umri ambao anaweza kukua zaidi hivyo ana matumaini hilo litafanikiwa akiwa huko ingawa anatakiwa kuzoea haraka mfumo wa Chelsea na kocha. Simeone amesema washambuliaji wakubwa huwa wanakuja na kuondoka Atletico na timu hiyo imekuwa ikifanikiwa kwenda mbele pamoja na kuondokewa na wachezaji wake wakubwa akiwatolea mfano kina Fernando Torres, Diego Forlan, Sergio Aguero, Radamel Falcao na sasa Diego Costa na David Villa.
No comments:
Post a Comment