Wednesday, January 7, 2015

PODOLSKI AANZA KWA SARE INTER.

MSHAMBULIAJI nyota wa Arsenal ambaye yuko kwa mkopo Inter Milan, Lukas Podolski ameitumikia timu hiyo kwa mara ya kwanza akitokea benchi katika kipindi cha pili wakati wakitoa sare ya bao 1-1 dhidi ya vinara wa Serie A Juventus. Walikuwa ni Juventus ndio waliotanguliwa kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Carlos tevez lakini bao hilo lilisawazishwa katika kipindi cha pili na Mauro Icardi baada ya Podolski kuingia muda mchache. Katika mchezo huo Mateo Kovacic wa Inter alipewa kadi nyekundu katika dakika za lala salama lakini Juventus walishindwa kupata bao la ushindi pamoja na upungufu wa wapinzani wao. Sare hiyo sasa inamaanisha kuwa Juventus wanaongoza Serie A kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Roma wanaowafuata kwa karibu ambao walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Udinese jana.

No comments:

Post a Comment