Friday, December 18, 2015

BARCELONA KUKWAANA NA MAHASIMU WAO WA CATALUNYA, ESPANYOL.

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mfalme, Barcelona wamepangwa kucheza na mahasimu wao jiji Espanyol katika hatua ya timu 16 bora ya michuano hiyo wakati Cadiz ambao waliingia hatua hiyo kufuatia kuenguliwa kwa Real Madrid wao watapambana na Celta Vigo. Mara ya mwisho Barcelona kukwaana na Espanyol katika michuano hiyo ilikuwa msimu wa mwaka 2008-2009 wakati huo wakinolewa na Pep Guardiola ambapo waliwafunga mahasimu wao hao jumla ya mabao 3-2 na kusonga mbele mpaka kunyakuwa taji. Cadiz waliopoteza mchezo wa mkondo wa kwanza katika hatua ya timu 32 bora kwa kufungwa mabao 3-1 na Madrid, walibahatika kusonga mbele baada ya timu hiyo kutolewa kutokana na kuchezesha mchezaji asiyeruhusiwa. Mechi zingine katika ratiba hiyo zitawakutanisha Sevilla dhidi ya Real Betis, Atletico madrid dhidi ya Rayo Vallecano, Athletic Bilbao dhidi ya Villarreal na Valencia wanaonolewa na Gary Neville watachuana na Dranada. Nyingine ni Mirandes dhidi ya Deportivo La Coruna na Eibar watakaoivaa Las Palmas.

No comments:

Post a Comment