Monday, December 7, 2015

HATMA LIGI YA MABINGWA IKO MIKONONI MWETU - RAMSEY.

KIUNGO wa Arsenal, Aaron Ramsey amesisitiza kuwa hatma yao katika michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya iko mikononi mwao wakati wakijiandaa kukwaana na Olympiakos ya Ugiriki katika mchezo wao wa mwisho wa makundi. Arsenal wanatofautiana alama tatu na Olympiakos wanaoshika nafasi ya pili na watalazimika kupata ushindi wa mabao 2-0 au kushinda zaidi ya mabao matatu katika mchezo wao wa Jumatano kama wanahitaji nafasi ya kusonga mbele. Ramsey ambaye kikosi chao kilipoteza mechi zao mbili mwanzo, anaamini kuwa wataweza kutengeneza nafasi na kuwataka wachezaji wenzake kuhakikisha wanazitumia vyema pindi wazipatapo. Kiungo huyo amesema hakuna lisilowezekana, kwani wana kikosi kikosi kizuri kinachoweza kupata matokeo wanayohitaji kama wakijituma kwa bidii.

No comments:

Post a Comment