Monday, December 7, 2015

LUKAS PODOLSKI USO KWA USO NA FLOYD "MONEY" MAYWEATHER.

MSHAMBULIAJI wa Galatasaray, Lukas Podolski ameonyesha kufurahishwa kupata nafasi ya kukutana na bingwa wa zamani wa dunia asiyepigika Floyd Mayweather. Nyota huyo wa zamani wa Arsenal alimkaribisha bondia huyo wa Marekani jijini Instabul wakati Mayweather akiendelea kufurahia muda wake nje ya ulingo. Podolski alituma picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa na Mayweather iliyoendana na ujumbe wa kusifia ujio wake huo nchini Uturuki. Mayweather ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Urusi, ametua Istanbul kukutana na mmiliki wa kampuni ya Brothers 4 Life-B4L, Umit Akbulut kwa ajili ya mazungumzo na kibiashara na mapumziko binafasi.

No comments:

Post a Comment