OFISA mkuu wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA, Martin Glenn amesema kuna uwezekano mkubwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Roy Hodgson kuendelea na kibarua chake hicho mpaka michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018. Hodgson aliajiriwa mwaka 2012 na mkataba wake unatarajiwa kumalizika baada ya michuano ya Euro mwakani. Akihojiwa Glenn amesema kama wakifanya vyema katika michuano ya Euro, haitakuwa na shaka kuwa Hodgson ndiye atakuwa mtu sahihi kwa ajili ya kuwapeleka katika michuano ya Kombe la Dunia. Glenn aliendelea kudai kuwa hana shaka kwamba watafanya vyema katika michuano hiyo ambayo itafanyika majira ya kiangazi mwakani, kutokana na kikosi imara cha wachezaji vijana walichonacho.

No comments:
Post a Comment