GOLIKIPA wa Leicester City, Kasper Schmeichel amesema amechoshwa na watu kumfananisha na baba yake Peter. Peter Schmeichel alikuwa golikipa nguli wa Manchester United akiwa ameshinda mataji matano ya Ligi Kuu, matatu ya FA na moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu nane aliyoichezea klabu hiyo. Mtoto wake huyo, Kasper amefuata nyayo za baba yake na ametumia muda wake wote wa kucheza soka akiwa kipa nchini Uingereza lakini amesema amechoshwa na watu kumfananisha na baba yake. Akihojiwa Kasper amesema kila mwezi anazidi kuchoshwa na suala hilo kwani alidhani ni suala la kupita lakini kadri siku zivyokwenda ndio linazidi. Kasper amesema baba yake pia anachukizwa na suala hilo, kwani kwa umri alionao sasa haipendezi tena kufananishwa na mtu.

No comments:
Post a Comment