Monday, December 7, 2015

KASHFA NYINGINE NZITO YA MAMILIONI YA DOLA YAMNYEMELEA BLATTER.

KIPINDI maalumu cha uchunguzi BBC, Panorama, kimeona ushahidi kwamba rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter aliyesimamsishwa kwa muda anachunguzwa na Shirika la Ujajusi la Marekani-FBI. Kampuni ya masoko ya michezo inaaminika kulipa mamilioni ya dola za Kimarekani kwa maofisa waandamizi wa FIFA katika miaka ya mwishoni mwa 1990 ili kupewa haki ya kutangaza michuano ya Kombe la Dunia. Aliyekuwa ameshikilia nafasi hiyo kabla ya Blatter, Joao Havelange, alikuwa ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo. Blatter, amekana kuwa na taarifa yoyote ya sakata hilo, lakini kipindi cha Panorama kimeona barua iliyosainiwa na Havelange ikieleza kuwa Blatter ana taarifa kamili.

No comments:

Post a Comment