Monday, December 7, 2015

PORTLAND TIMBERS MABINGWA WAPYA WA MLS.

TIMU ya Portland Timbers wametawadhwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Marekani-MLS kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Columbus Crew katika mchezo wa fainali huku beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza Liam Ridgewell akilibeba taji hilo. Katika mchezo huo Timbers walishinda kwa mabao 2-1 ambayo yalifungwa na Diego Valeri pamoja na Rodney Wallace katika kipindi cha kwanza huku lile la kufutia mchozi la Columbus likifungwa na Kei Kamara. Nahodha wa Timbers Ridgewell mwenye umri wa miaka 31, amewahi kucheza katika timu za Ligi Kuu zikiwemo Aston Villa, Birmingham City na West Bromwich Albion. Ushindi huo unaifanya Timbers kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka alipojiunga na MLS mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment