Tuesday, December 8, 2015

MESSI AMTUMIA RONALDINHO JEZI YENYE SAINI YAKE KUMKUMBUKA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amemtumia fulana yenye saini yake Ronaldinho ikiwa kama ishara ya kumkumbuka mchezaji mwenzake huyo wa zamani. Kabla ya Messi kuitwaa fulana yenye namba 10 mgongoni, ilikuwa ikivaliwa na nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Brazil. Messi alitengeneza ukaribu wa kipekee na Ronaldinho wakati alipoibuliwa kwa mara kwanza katika kikosi cha kwanza mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 16. Zawadi hiyo ni kwa ajili ya kipindi maalumu cha Barca TV kitakachoonyeshwa wakati wa Christmas, kusheherekea miaka 10 ya ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Real Madrid ambao ulishuhudia mashabiki wa upinzani wakimpa heshima Ronaldinho kwa kiwango alichoonyesha katika mchezo huo. Ronaldinho ameonyesha kufurahishwa na zawadi hiyo aliyotumiwa na Messi kwa kumshukuru na kumpongeza kwa jitihada zake kubwa alizoonyesha mpaka kufikia hadhi aliyonayo sasa.

No comments:

Post a Comment