MENEJA wa Juventus, Massimiliano Allegri amekitaka kikosi chake kujifunza pamoja na kupata nafasi ya kucheza fainali ya Kombe la Italia. Wakiwa wanaongoza kwa mabao 3-0 ushindi waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza, vinara hao wa Serie A walijikuta wakilazimishwa matuta na Inter Milan katika mchezo wa marudiano kabla ya kushinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-3 katika Uwanja wa San Siro jana. Allegri amesema vijana wake wanapaswa kujifunza kutokana na mchezo huo ambao uliokuwa ukionekana kama umekwisha baada ya ushindi wa kwanza waliopata. Meneja aliendelea kudai kuwa mechi kama hiyo ndio ya kujifunza kwani wanaweza kujitengenezea naafsi nzuri lakini haimaanishi kama kila kitu kimekwisha.
No comments:
Post a Comment