Thursday, March 3, 2016

CECH, KOSCIELNY KUIKOSA SPURS.

KLABU ya Arsenal inatarajia kuwakosa Petr Cech na Laurent Koscielny katika mchezo wao muhimu wa Jumamosi hii dhidi ya mahasimu wao kutoka kaskazini mwa jiji lam London Tottenham Hotspurs. Koscielny alikosa mchezo wa jana ambao walifungwa na Swansea City kutokana na matatizo ya kifundo cha mguu na hatarajiwi kupona kwa wakati kwa ajili ya mchezo dhidi ya Spurs. Golikipa Cech yeye alipata majeruhi ya msuli wa paja dakika za majeruhi katika mchezo dhidi ya Swansea jana usiku. Akizungumza na wanahabari meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alithibitisha Cech kuumia kwa Cech na kudai kuwa hatacheza katika mchezo dhidi ya Spurs na nafasi yake itachukuliwa na Ospina.

No comments:

Post a Comment