Friday, March 18, 2016

AUBAMEYANG ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA BABU YAKE.

MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang ametuma salama za rambirambi kufuatia kifo cha babu yake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 waliopata timu yake dhidi ya Tottenham Hotspurs katika michuano ya Europa League. Dortmund walikuwa tayari wakiongoza kwa mabao 3-0 ushindi waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza lakini walijihakikishia nafasi yao ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo kwa kupata ushindi mwingine jijini London. Aubameyang aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akieleza ugumu wa kucheza huku akifahamu babu hayuko naye tena na kumpa zawadi ya mabao mawili aliyofunga. Nyota huyo wa kimataifa wa Gabon amekuwa katika kiwango bora msimu huu baada ya kufunga mabao 35 katika mechi 40 alizocheza katika mshindano yote.

No comments:

Post a Comment