Friday, March 18, 2016

GUARDIOLA AAGIZA CITY WAMUUZE KOMPANY.

VYOMBO vya habari nchini Uingereza vimedai Pep Guardiola amewataka Manchester City kumuuza Vincent Kompany majira ya kiangazi. Taarifa zinadai kuwa Guardiola tayari amefanya mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa City Txiki Begiristain na yuko tayari kumuuza nahodha huyo wa klabu ili aweze kusuka sfu nyingine mpya ya ulinzi. Guardiola pia anadaiwa kumuwania beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte kama mbadala wa Kompany. Kompany ameichezea City mechi 13 pekee msimu huu kutokana na majeruhi ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakimsumbua.

No comments:

Post a Comment