Thursday, March 17, 2016
BARCELONA WANAFANYA MAISHA YA KAWAIDA KUWA SANAA - WENGER.
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema Barcelona wana wachezaji wawili au watatu ambao wanageuza maisha ya kawaida kuwa sanaa. Arsenal walieunguliwa katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa sita mfululizo baada ya kufungwa jumla ya mabao 5-1 na Barcelona katika mechi mbili walizokutana. Washambuliaji mahiri wa Barcelona Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez wote walifunga mabao katika ushindi wa mabao 3-1 waliopata jana. Akihojiwa Wenger amesema wamekuwa mahiri kwa ubunifu wa hali ya juu pindi wanapofikia hatua ya mwisho ya kushambulia.
Meneja huyo aliendelea kudai kuwa pamoja na hayo lakini anadhani kikosi chake pia kilicheza kwa umahiri na kutengeneza nafasi kadhaa hatari ambazo walishindwa kuzitumia vyema.
No comments:
Post a Comment