Tuesday, March 15, 2016

POGBA ADAI KUWAHUDU RONALDO NA ZIDANE.

KIUNGO wa mahiri wa kimataifa wa Ufaransa na Juventus, Paul Pogba amewachagua mshambuliaji wa zamani wa Brazil Ronaldo na meneja wa sasa wa Real Madrid Zinedine Zidane kuwa watu waliowahusudu sana wakati akikua. Nyota huyo ambaye amefikisha miaka 23 leo, anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora chipukizi Ulaya na anatarajiwa kuwa mtu muhimu katika kikosi cha Ufaransa kitakachokuwa kikipigania kushinda taji la Ulaya katika ardhi yao kiangazi hiki. Mara ya mwisho Ufaransa kuandaa michuano mikubwa ilikuwa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1998 wakati Brazil iliyokuwa na Ronaldo ilipofungwa katika fainali na nchi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Zidane. Pogba amebainisha kuwa Ronaldo na Zidane wameacha alama kubwa kwa upande wake na wamemsaidia kuwa mchezaji aliye hivi sasa.

No comments:

Post a Comment