Tuesday, March 15, 2016

CAPELLO AMUONYA CONTE ASITEGEMEE MTEREMKO KAMA AKIENDA CHELSEA.

MENEJA wa zamani wa Uingereza, Fabio Capello amemuonya Antonio Conte kuwa atarajie utamaduni tofauti pindi anatakapokubali kibarua cha kuinoa Chelsea msimu ujao. Shirikisho la Soka la Italia tayari limeshathibitisha kuwa Conte ataachia ngazi kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya michuano ya Euro 2016 na kuna mategemeo makubwa ya kwenda kumpokea mikoba Guus Hiddink kule Stamford Bridge. Tetesi zinadai kuwa meneja huyo mwenye umri wa miaka 46 atapewa mkataba wa miaka mitau baada ya mazungumzo na Chelsea kuendelea vyema. Mara ya mwisho akiwa Juventus, Conte aliiongoza kunyakuwa mataji matatu mfululizo ya Serie A kabla ya kujiuzulu Julai mwaka 2014 na kwenda kuchukua nafasi ya Cesare Prandelli katika kikosi cha Italia. Akihojiwa Capello amesema kama Conte akikubali kuinoa Chelsea anapaswa kuleta mafanikio ya haraka ili kutoingia katika mzozo na mmiliki wake Roman Abramovich. Capello aliendelea kudai kuwa Chelsea hawawezi kumlinda kama ilivyokuwa Juventus na kama Abramovich akikununulia wachezaji watano au sita huwezi kumaliza katika nafasi ya tano akakuvumilia.

No comments:

Post a Comment