Friday, March 4, 2016

BARCELONA WAWEKA REKODI MPYA HISPANIA.

KLABU ya Barcelona imefanikiwa kuweka rekodi mpya nchini Hispania kwa kucheza mechi 35 bila kufungwa katika mashindano yote baada ya kuifunga Rayo Vallecano jana usiku. Mabingwa hao wa Hispania ambao wanaongoza La Liga, waliifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa kwa kipindi kirefu na mahasimu wao Real Madrid Jumapili iliyopita wakati walipoifunga Sevilla kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Camp Nou. Madrid walikuwa wakishikilia rekodi hiyo toka msimu wa 1988-1989 wakati wakiwa na nyota kama Hugo Sanchez na Emilio Butragueno ambapo walishinda mechi 25 na kutoa sare tisa. Hata hivyo Barcelona mbali na kuivunja rekodi hiyo lakini pia wameiboresha kwani wao wameshinda mechi 29 na kutoa sare mechi sita pekee. Katika mchezo wa jana Rayo walionekana wepesi kwa Barcelona baada ya kuchapwa mabao 5-1 huku Lionel Messi akifunga hat-trick.

No comments:

Post a Comment