Friday, March 4, 2016

HODGSON MBIONI KUMUITA RASHFORD KATIKA KIKOSI CHA EURO 2016.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amedai kuwa anaweza kumuita chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford katika kikosi chake atakachokitumia katika michuano ya Euro 2016. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ameonyesha kiwango kikubwa wiki iliyopita katika mechi za kwanza chini ya meneja wa United Louis van Gaal. Akiwa tayari ameshatajwa katika vikosi vya nchi hiyo kwa vijana chini ya umri wa miaka 16 na 18, Hodgson amedai sasa yuko tayari kumuita katika kikosi cha wakubwa. Akizungumza katika semina ya makocha iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Hodgson amesema angependa zaidi watu kutompa shinikizo chipukizi huyo kwani bado anahitajika kuimarika zaidi. Hodgson aliendelea kudai kuwa amekuwa akimfuatilia Rashford kwa miaka miwili sasa na tayari yuko katika mipango yao.

No comments:

Post a Comment