MSHAMBULIAJI Inter Milan Mauro Icardi anaweza kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu baada ya klabu hiyo kuthibitisha kuwa alipata majeruhi ya goti. Icardi alipata majeruhi hayo Jumamosi iliyopita katika mchezo wa Serie A dhidi ya Bologna ambapo Inter walishinda mabao 2-1. Klabu hiyo ilithibitisha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter na kudai kuwa ataukosa mchezo wao wa mwishoni mwa wiki hii dhidi ya mahasimu wao As Roma. Icardi ameshafunga mabao 12 katika mechi 26 za Serie A na kuifanya Inter kushikilia nafasi ya tano katika msimamo.
No comments:
Post a Comment