KLABU ya Manchester United haitaadhibiwa na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA baada ya baadhi ya mashabiki wake kuimba nyimbo za kejeli kuhusiana na janga la Hillsborough katika mchezo wa Europa League dhidi ya Liverpool Alhamisi iliyopita. Kiungo wa United Marouane Fellaini pia ameepuka adhabu kufuatia tuhuma za kumpiga kiwiko Emre Can katika dakika za mwisho za mchezo. UEFA imeamua kutochukua adhabu yeyote kutokana na matukio hayo kutotajwa katika tarifa ya waamuzi. Liverpool walifanikiwa kushinda mabao 2-0 katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza hatua ya 16 bora na marudio yanatarajiwa kuwa Alhamisi hii katika Uwanja wa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment