KLABU ya Barcelona imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya alama 11 kufuatia kushinda mchezo wao dhidi ya Eibar jana. Katika mchezo huo Barcelona ilishinda kwa mabao 4-0 ambayo yalifungwa na Lionel Messi aliyefunga mawili huku Luis Suarez na Munir El Haddadi wakifunga bao moja kila mmoja. Messi sasa anakuwa amefikisha mabao 21 msimu huu huku Barcelona wakiongeza rekodi yao ya kutofungwa kufikia mechi 36. Washambuliaji nyota watatu wa timu hiyo Messi, Suarez na Neymar kwa pamoja sasa wanakuwa wamefikisha jumla ya mabao 100 katika mshindano yote msimu huu.
No comments:
Post a Comment